Saturday, October 12, 2013




Utafanya nini uko kwenye ndege ndogo alafu Rubani akazimia na hujui kuendesha? imemkuta huyu mzee


John 1






Hii imetokea kwa huyu Mzee wa miaka 77 John Wildey huko Uingereza ambae pamoja na kufanikiwa kuishusha ndege mpaka ardhini anasema yeye sio shujaa bali wale waliokua wanampa moyo wakati akiwa hajui afanye nini ndio mashujaa.
Anakwambia ‘tukiwa angani Rubani ambae ni rafiki yangu alijisikia vibaya ghafla na kuzimia kutokana na mshtuko wa moyo hivyo nikafikiria kuwa lazima nichukue usukani niendeshe lakini sikuwa nafahamu ninachopaswa kufanya hivyo nikaita radio call ili nipate msaada’ – John
john 4Wakati huo akiwa hewani tayari vikosi vya uokoaji pamoja na Ambulance vilikua vimejipanga uwanjani tayari kwa lolote.
‘Helicopter ilinifata kutoa msaada wa jinsi ya mimi kutua nikawa nafata maelekezo yao kiukweli nilikua sijui nibonyeze nini na nilipojaribu kutua sikuweza kuona barabara ya kutua hivyo ilishindikana japo baadae baada ya majaribio kadhaa iliwezekana kutua, nilitua kwanza na tairi la mbele lakini cha kusikitisha rubani alikua amefariki, familia yake iliomba jina la Marehemu lisitajwe popote hata na Polisi’ – John

No comments:

Post a Comment