Tuesday, October 29, 2013

AJALI MBAYA YATOKEA MLIMA WA MZALENDO IGAWILO JIJINI MBEYA...!!


 
Lori baada ya kupata ajali katika eneo la mlima wa Mzalendo Igawilo jijini Mbeya wakati likielekea jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo wakipelekwa hospitali.

UKATILI: BABA ATUMIA PANGA NA RUNGU KUMWADHIBU MWANAYE KWA KOSA LA KUKATAA KWENDA SHULE HUKO MBEYA..!!

Victoria Mukama (10) baada ya matibabu


Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.


 Victoria Mukama (10) baada ya matibabu



KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama  mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.

Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.

Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.

Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya matibabu.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.

Alisema alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.

Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.

Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka kumuokoa.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa ndani ya jamii.

Aliongeza kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa pamoja na kuchangia mada.

Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.

Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.

Sunday, October 27, 2013

UKIATILI! BABA NA MAMA WAGOMBEA MTOTO,BAADA YA BABA KUZIDIWA NGUVU NA MKEWE ALIPUA WATOTO KWA PETROLI...

Mtoto aliyefariki Mtoto Matrida Michael mwenye umri wa miaka 9, mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Oktoba 23, mwaka huu kufuatia majeraha ya moto aliyoyapata. Marehemu Matrida na watoto wenzake wawili, Tatu Mapunda (9) na Flora Mapunda (7), waliungua moto Oktoba 16, mwaka huu saa tano usiku wakiwa wamelala baada ya chumba chao kulipuliwa kwa petroli na mtu anayedaiwa kwa ni Brighton Mnamwa. Inadaiwa kwamba chanzo cha Mnamwa kuamua kulipua watoto hao ni ugomvi baina yake na mkewe Janeth Lwena, waliyekuwa katika mzozo wa kumgombea mtoto wao wa miaka mitatu aitwaye Tulizo. Watoto ambao wako hoi Mama mdogo wa marehemu Mary Ivo ambaye alikuwepo msibani hapo, alisema kwamba dada yake yupo Muhimbili anawauguza majeruhi wawili waliobakia na kwamba wakati wa ugomvi wao, mke alimzidia nguvu mumewe. Aidha aliendelea kueleza kwamba baada ya mke kumzidi nguvu, mume alizusha ugomvi mkubwa huku akitishia kumuua kwa panga, hata hivyo mke alimdhibiti. ‘Baadaye mume huyo inadaiwa kwa aliondoka hapo nyumbani na haikujulikana alikoenda, ndipo mke alienda chumba cha jirani na kumuomba Matrida abakie na watoto pale chumbani akatoe taarifa polisi lakini mtoto aliyekua akigombewa alienda naye kituoni,’ alisema mama mdogo. Habari zinasema kwamba yule mume alienda kituo cha mafuta kununua petroli ili aweze kuwatekezeza wote, lakini hakujua kama mkewe pamoja na mtoto aliyekua akigombewa hawakuwepo. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba baada ya mume huyo kurudi, alimimina mafuta hayo katika chumba hicho kisha kukilipua wakati watoto hao watatu wakiwa katika usingizi na wananchi walipojitokeza walikuta chumba kikiteketea huku sauti ya watoto ikisikika wakiomba msaada. Wananchi waliokuwepo kwenye eneo la tukio walisema kwamba walipatwa na uchungu hivyo walijitosa kuuzima moto ule na kuwaokoa watoto hao watatu huku wakiwa wameungua vibaya, waliwakimbiza Hospitali ya Temeke na kutokana na hali yao kuwa mbaya walipelekwa Muhimbili ambapo Matrida alifariki dunia. Naye Michael Melkiori Kess, baba wa marehemu alisema kwamba amesikitishwa na kitendo hicho na amedai ni cha kinyama hivyo ameiomba dola kumsaka mtu huyo hatari kwani huko aliko kwa sasa bado anaweza kusababisha majanga megine. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtoni Sabasaba, Mwita Mang’ana alisema kwa kitendo hicho ni cha kinyama kwani amesababisha kujeruhi watoto wasiokua na hatia na amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapatikana . Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba msako wa kumtafuta mtuhumiwa unaendelea sambamba na uchunguzi wa tukio. chanzo boss ngasa

Friday, October 25, 2013

Kuhusu Marekani kufatilia kwa siri simu ya mkononi ya Kansela wa Ujerumani


Angela MKwenye headlines za dunia sasa hivi miongoni mwa stori kubwa ni hii ya madai ya Ujerumani kwamba Marekani imekua ikifatilia kwa siri mazungumzo ya simu ya Ujerumani Kansela Angela Merkel ambapo kwa mujibu wa DW Swahili, Ujerumani imemuita balozi wa Marekani nchini humo John B. Emerson kuzungumzia madai  hayo ya Idara ya usalama wa kitaifa ya Marekani kuyafatilia mawasiliano ya simu ya mkononi ya kansela.
Hii stori imekuja wakati Merkel na viongozi wengine wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kwa mkutano ambao unaonekana utagubikwa na habari za mawasiliano ya siri yanayodaiwa kufanywa na Marekani kwa washirika wake ambapo waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Thomas de Maiziere aliliambia shirika la habari la ARD  Ujerumani kwamba iwapo madai haya yatathibitishwa kuwa ya kweli basi litakuwa ni jambo baya sana.
De Maiziere amesema Marekani itabakia kuwa rafiki wa Ujerumani lakini jambo linalodaiwa kufanywa sio sahihi kabisa baada ya kupokea taarifa kwamba Marekani ilifatilia mawasiliano ya kansela Angela Merkel hatua iliomfanya Merkel mwenyewe Jumatano kumpigia simu mara moja rais wa Marekani Barack Obama kutaka ufafanuzi zaidi kwa sababu aliamini kuna siku mawasiliano yake yatafatiliwa lakini sio na Marekani.
Baada ya haya madai ya Ujerumani, Marekani imekanusha kwa kusema haijayachunguza mawasiliano ya Kansela na haiwezi kufanya hivyo kamwe.
ANGELA M 2Haya madai yalitolewa kwa mara ya kwanza na mfanyakazi wa zamani wa idara ya kitaifa ya usalama nchini Marekani, NSA, Edward Snowden yaliyochapishwa na jarida la habari la Ujerumani, Der Spigel na sasa yameanza kuleta uhusiano mbaya kati ya Marekani na mataifa ya Ulaya yaliyokasirishwa na habari hizo za kufanyiwa uchunguzi wa siri na mshirika wao.
Mpaka usiku wa October 24 2013, taarifa mbalimbali ziliripoti kwamba mpaka sasa imefahamika ni viongozi wa  nchi 35 kubwa wameshafatiliwa kwenye mawasiliano yao ya simu za mkononi bila wenyewe kufahamu.
    chanzo millad ayo

Monday, October 21, 2013

ASKARI WA HIFADHI WAUA MBELE YA KITUO CHA POLISI





 
NA DANIEL LIMBE
Askari wa Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo wilayani 
Geita mkoani hapa, wamekumbwa na kashfa nyingine
 baada ya kudaiwa kumuua raia mmoja kwa kipigo 
mbele ya kituo kidogo cha polisi Chato.
Aliyeuawa ametambulika kuwa ni Moshi Nkola
 (39), mkazi wa kijiji cha Mkuyuni kata ya
 Chato wilayani hapa.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Pudensiana Protas,
 alidai kutokuwa na taarifa ya tukio hilo na kuahidi kufuatilia
 ukweli wa jambo hilo kutoka kwa wasaidizi wake.
Akielezea tukio hilo, kaka wa marehemu, Paulo Nkola (42),
 aliliambia NIPASHE Jumapili kuwa nduguye alipigwa na 
askari wawili wa hifadhi ya kisiw
a cha Rubondo (hakuwataja majina) Oktoba 17, majira 
ya saa 4 usiku wakati akitoka kwenye duka la kuuza pombe.

Alisema kabla ya kipigo hicho, Nkola alikuwa akiendesha 
pikipiki yake wakati akirejea nyumbani kwake na baadaye
 alikutana na askari hao wakamtaka awabebe kwenye pikipiki
hiyo kwa nguvu kwa lengo la kuwapeleka kwenye mwalo wa
 kasenda ambapo kuna ghati la kuvukia ili kuingia ndani ya
 hifadhi hiyo.
Baada ya kukaidi amri ya askari hao, mmoja wao alipanda
 kwa makusudi wakati Nkola akitaka kuondoka eneo hilo, 
hali iliyosababisha kuyumba na kuanguka. Kitendo hicho 
kilichowaudhi askari hao na kuanza kumshambulia kwa kipigo.
Paulo alisema baada ya mdogo wake kuzidiwa nguvu, alilazimika
 kukimbilia kituo kidogo cha polisi cha Muganza ili kunusuru
 maisha yake, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida watu hao 
walimfuata mpaka kituoni hapo na kuendelea kumpiga mbele ya 
askari wa polisi waliokuwa zamu.
Kutokana na kipigo hicho, Nkola alijeruhiwa vibaya na baadaye
 kuomba PF3 kwa ajili ya matibabu kwenye zahanati ya 
Nyabugera iliyopo kata ya Muganza.
Hata hivyo, baada ya hali ya Nkola kuonekana kuzidi kuwa 
mbaya, alilazimika kwenda hospitali ya wilaya ya Chato ili
 kupata huduma zaidi kabla ya kukumbwa na mauti hayo
 usiku wa kuamkia jana.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Mashaka Majige, maarufu
 kwa jina la Kishimba, alisema askari hao pia walikuwa wamelewa
 pombe ambapo walimtaka Moshi awabebe kwenye pikipiki kwa
 nguvu ambapo alikaidi amri hiyo.
Alisema hata baada ya merehemu kukimbilia kituo cha polisi na
 kuingia ndani, askari hao walimfuata na kumshambulia mbele
 ya askari waliokuwepo bila kuwazuia.
Diwani wa kata ya Muganza, Marco Maduka, amekiri kutokea 
tukio hilo na kudai kuwa askari hao walikuwa wametoka kwenye 
hifadhi ya kisiwa cha Rubondo na kwamba walionekana wakinywa
 pombe kabla ya kufanya ukatili huo.
Alidai kuwa askari hao ambao majina yao hayajafahamika mara 
moja, walimpiga mtu huyo ndani ya kituo cha polisi kabla ya
kukumbwa na mauti.
Jeshi la polisi wilayani hapa limekiri kuwapo kwa madai hayo 
na uchunguzi unafanyika. Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na
 mauaji hayo.
NIPASHE Jumapili lilipomtafuta Ofisa doria mkuu wa hifadhi ya
 kisiwa cha Rubondo, aliyefahamika kwa jina moja la Chuwa ili
 kuzungumzia tuhuma hizo simu yake haikupatikana.
Mganga mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Chato, Dk. Pius Buchukundi,
 alikiri kupokelewa kwa Nkola akiwa mgonjwa lakini wakati akipatiwa
 matibabu alipoteza maisha.
Uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa Nkola aliumia kichwa
 kutokana na kitu kisichojulikana kumgonga na kusababisha kupasuka
 baadhi ya mishipa iliyosababisha damu nyingi kuvuja eneo la jicho.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Thursday, October 17, 2013

MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA Labels: MAKALA


Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. 
Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ naSteven Kanumba ‘The Great’.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda.
VIFO MILIONI 605
Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini.
Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao.

Steven Kanumba. 

WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU
Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kundi la Five Stars wapatao 14, Kanumba, Sharo Milionea na mwanamuziki James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’.
Pia alidai kuwa alihusika katika vita kati ya aliyekuwa Rais wa Iraq, Sadam Hussein na Marekani kwa kutumia pepo la uchonganishi alilolitaja kwa jina la ‘Magweju’.
Pia mchungaji huyo alidai kuhusika na shambulio la hivi karibuni la Al-Shabaab katika maduka ya Westgate la Nairobi nchini Kenya na matukio mengine mengi hadi kufikia idadi hiyo ya vifo vya watu milioni 605.

Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’. 

AWAONEA HURUMA WASANII, AWAONYA
Mchungaji huyo aliendelea kusimulia kuwa alipokuwa katika ulimwengu wa giza aliwahi kuwaonea huruma wasanii kama Kanumba, Sharo Milionea na Mtoto wa Dandu na kuwatokea kimiujiza akiwaonya waokoke kabla ya kuchukua roho zao huku mashabiki wao wakibaki na simanzi wakiamini kuwa vifo vyao ni vya kawaida.
Alidai kuwa baada ya kuwafuata mastaa hao na kuwaonya walikataa na badala yake akawaua.
Akiendelea kulishuhudia kanisa, Mchungaji Mayanga alisema kuwa kwa sasa ameokoka na kuachana na mambo ya giza, hivyo haogopi kuzungumza ukweli kwa kuwa roho wa Bwana anamuongoza kushuhudia kila kitu alichokifanya ili waumini watambue uwezo wa Mungu.

Gari la Sharo baada ya ajali. 
ANA SIRI NZITO ZA VIGOGO
Huku akiomba hifadhi ya majina ya wahusika, mchungaji huyo alihitimisha ushuhuda wake kwa kudai kuwa ana siri nzito za vigogo au watu wakubwa ambao aliwahi kwa namna moja au nyingine kuwapa utajiri wa nguvu za giza.
UTABIRI
Hata hivyo, baadaye jamaa huyo alijitabiria kuwa atakamatwa na kufungwa siku moja kutokana na siri alizonazo.
“Yaani nina siri za watu wengi sana, nikiwaambia mtaogopa na nchi itatikisika. Najua siku moja watu watanikamata na kunifunga pingu kwa siri nilizonazo, lakini kamwe siogopi kwa kuwa Bwana ananiongoza,” alisema Mchungaji Mayanga.

Jeneza la Kanumba. 


KANUMBA, SHARO MILIONEA
Kanumba alifariki dunia mwaka jana akiwa nyumbani kwake Sinza-Vatican, Dar huku Sharo Milionea akipoteza uhai kwenye ajali ya gari iliyotokea wilayani Muheza, Tanga wakati msanii huyo akienda kwao mkoani humo akitokea Dar.

PICHA 9 JINSI WATUHUMIWA WA UGAIDI MSITUNI WALIVYOPELEKWA MAHAKAMANI LEO MTWARA





Polisi walijua kabisa msafara wao utakua umewabeba watuhumiwa waliokamatwa kwenye mafunzo ya kijeshi ambayo yalikua yanatolewa kupitia CD za Al Qaeda na Al Shabaab hivyo wakajiandaa kwa ukubwa huu

Taarifa ambazo zimeifikia millardayo.com ni kwamba wale watuhumiwa wa ugaidi waliokamatwa wakifanya mazoezi msituni 88.4 Mtwara, walipelekwa Mahakamani asubuhi ya leo October 17 2013 lakini kutokana na baadhi ya taratibu za kimahakama ikashindikana kupandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mtwara hivyo wakarudishwa mahabusu
mpaka hapo itakapoamuliwa ni siku gani wapelekwe tena Mahakamani.

Mwanzoni walikua wamekamatwa 11 tu lakini taarifa nyingine zilizoifikia millardayo.com zinaamplfy kwamba idadi imeongezeka baada ya wengine wawili kukamatwa kulekule walikokamatiwa wengine ambapo hawa wawili hawakukutwa na silaha wala kingine chochote kama ilivyotokea kwa wale wa mwanzo ambao walikutwa na mapanga, silaha mbalimbali pamoja na CD za DVD ambazo zinamafunzo ya kijeshi ya Al Shabaab na Al Qaeda.

Wawili hawa wamekiri kwamba mwalimu wao kule msituni alikua akiwapa mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo kupiga karate, utumiaji wa silaha ambapo pia walikua wakiishi hukohuko msituni kwenye Mapango.



Endelea kukaa karibu na millardayo.com na pia unaweza kujiunga kuwa mwanafamilia kupitia facebook.com/millardayo twitter.com/millardayo na instagram.com/millardayo ili kuwa wa kwanza kupata Breaking news, matukio ya michezo, muziki, movie na mengine mbalimbali.







Hili hapa juu ndio gari lililobeba baadhi ya hao Watuhumiwa wa ugaidi.



Wednesday, October 16, 2013

MAJANGA!! MAITI YAFUKULIWA MAKABURINI NA KUKATWA KICHWA.....!!




HOFU imezidi kutanda miongoni mwa wakazi wa mji wa Geita, baada ya watu wasiojulikana kufukua kaburi, kisha kukata kichwa cha maiti iliyokuwemo na kuondoka nacho. Tukio hilo la kusikitisha na ambalo halipaswi kufumbiwa macho, lilitokea jana katika makaburi yaliyopo Mtaa wa Elimu Nyantorotoro, mkoani hapa.

Tukio hilo ambalo limeshuhudiwa na umati mkubwa, limekuja siku chache wakati wakazi wa mji huo wakiwa na hofu, baada ya kutokea tukio la mtoto Shaabani Maulidi (16), aliyefariki miaka zaidi ya miwili iliyopita na kuonekana akiwa hai jirani na mtaa huo.

Watu hao, ambao walipasua sanduku la maiti na baadaye kutoa kichwa cha maiti hiyo ya mwanamume ambayo jina lake halikufahamika, waliacha kaburi wazi bila kulifukia.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Elimu Nyankumbu, Hassan Malima, tukio hilo liligunduliwa saa tatu asubuhi na watu waliokwenda eneo hilo kuchimba kaburi, baada ya kutokea msiba kwa Mchungaji Mtafuten Mihana wa Kanisa la PEFA, aliyefiwa na mtoto wake, Rebeka (28).

"Tulipofika katika eneo hilo tukiangalia sehemu ya kuchimba kaburi kwa ajili ya huyo marehemu mtoto wa mchungaji, ndipo tukaona hilo kaburi likiwa limefukuliwa, tuliposogea tukashuhudia maiti ikiwa imekatwa kichwa," alisema mwenyekiti huyo.

Inasemekana kaburi hilo limefukuliwa majira ya usiku wa kuamkia jana na kwamba maiti iliyokuwemo inadaiwa kuwa imezikwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita, ingawa ndugu hawakujulikana kutambua hali hiyo.

Uongozi wa mtaa huo baada ya kupata taarifa za tukio hilo, linalohusishwa na imani za kishirikina, walitoa taarifa polisi, ambao walifika eneo la tukio, wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Geita (OCD), Bwire.

Polisi kwa kushirikiana na wananchi, walifukua kaburi hilo ili kutambua jinsia ya maiti hiyo, ambayo ilijulikana kuwa ni ya kiume.

Mchungaji wa Kanisa la PEFA katika mtaa huo, Mtafuten, alisema tukio hilo ni la imani za kishirikiana, kutokana na wananchi kukosa imani na kuamini kutumia njia hiyo wanaweza kufanikiwa katika maisha yao.

Alisema watu wamekosa imani ya Mungu na kwamba wanadiriki kuchukua viungo vya watu waliokufa na kuzikwa, hivyo amewataka watu kuachana na imani za kishirikina na badala yake wamtegemee Mwenyezi Mungu pekee watafanikiwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita (RPC), Leonard Paulo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kwamba uchunguzi bado unaendelea.

Tuesday, October 15, 2013

MIUJIZA:MTOTO ALIYEKUWA AMEFARIKI AOMBEWA NA KUFUFUKA....!!



Mtoto aliyefufuka (katikati) akiwa ameshikwa na Mch. Gwajima (kulia) na Mch. Costa (kushoto)

Ni jumapili tulivu katika viwanja vya kanisa jipya la Ufufuo na Uzima jijini Arusha; ambapo
Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Tanzania, Mch. Josephat Gwajima ameendelea na ziara yake mkoani humo kwa kuwafundisha viongozi wapya wa masomo ya kumtumikia Mungu maarufu kama Potential shepherd. Mwisho wa Ibada ya Asubuhi ambayo ilitawaliwa na mafundisho zaidi ilifungua pazia kwa ibada ya jioni ambayo ilikuwa ni fursa kwa wale ambao hawakuweza kuwepo asubuhi nao kushiriki.

Majira ya saa kumi kamili, sifa zilivuma na baadaye kufuatiwa na ukaribisho wa Mch. Gwajima kutoa neno la Uzima. majira ya saa kumi na mbili kasoro; akaingia mama mmoja katikati ya ibada akiwa amembeba mwanaye ambaye kwa muonekano wa awali alikuwa amelegea mwili wote yaani amekufa.
Mama huyo ambaye alikuwepo katika mafundisho ya asubuhi na kujiunga na mafundisho hayo ya potential shepherd; aliendelea kusema kuwa baada ya kuona mwanaye hapumui wala mapigo ya moyo hayasikiki hakuona msaada wa haraka zaidi ya kumkimbiza kanisani hapo Ufufuo na Uzima.


Aliingia kanisani wakati Mch. Josephat Gwajima akiwa anahubiri hivyo kupokelewa na Mchungaji Msaidizi aitwaye Yeconia Bihagaze ambaye alimuombea mtoto huyo palepale na muda mfupi uliofuata mtoto alifufuka kutoka kwa wafu. Mungu ameendelea kudhihirisha neno la Mchungaji Josephat Gwajima ndani ya jiji la Arusha hali inayosababisha maelfu ya watu kuingia na kutoka katika viwanja hivyo kwaajili ya maombezi.


Jackson Benty akiimba katika ibada kanisani hapo.
Hata hivyo GK ilipotaka kupata maelezo zaidi kuhusiana na mambo yalivyokuwa mpaka mtoto huyo kufikishwa madhabahuni, mwanahabari wetu kutoka Ufufuo hakupata nafasi ya kukutana na mama huyo kwa maelezo zaidi kutokana na mwanahabari wetu kutingwa na kazi nyingi za media kanisani hapo.


Mchungaji Gwajima akifundisha kanisani hapo. Picha na shuhuda zaidi tembelea 
          source skendo za mjini

DALALI WA NYUMBA AMBAKA MTOTO WA MIAKA SITA NA KUMJERUHI VIBAYA.....




Dalali wa viwanja na nyumba eneo la Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka sita na kumjeruhi vibaya sehemu zake za siri.
Tukio hilo limetokea Septemba 3, mwaka huu, ambapo mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alifanyiwa unyama huo na dalali huyo anayejulikana kwa jina moja la Mgosi.
Akizungumza kwa masikitiko na gazeti hili, mama mkubwa wa mtoto huyo, Elizabeth Aloyce (28), alisema Mgosi ambaye ni dalali wa viwanja na nyumba katika eneo hilo, alikuwa akimfanyia kitendo hicho kwa muda mrefu.
Alisema kugundulika kwa tabia hiyo chafu ilikuja baada ya mtoto huyo kushindwa kutembea kutokana na maumivu makali.
Elizabeth alidai kwamba siku ya tukio alirudi nyumbani mapema kutoka kwenye biashara zake, alipoingia ndani alimkuta mtoto huyo amelala huku akiugulia.
Alipomuuliza kitu gani anachoumwa, mtoto huyo alianza kulia huku akificha sehemu zake za siri.
"Nilishtuka sana kuona hali ile, nilimshika na kuanza kumchunguza ndipo nikagundua sehemu zake za siri zimeharibika na kibaya zaidi mbegu za kiume zilikuwa zimeenea kila mahali," aliongeza kusema.
Kutokana na hali hiyo, aliamua kuwaita majirani na baada ya kushuhudia walikiri mtoto huyo amebakwa.
Baada ya kugundua suala hilo walimbana mtoto huyo amtaje mtu aliyemfanyia kitendo hicho, ndipo alipomtaja jina la mtuhumiwa na kwamba ilikuwa siyo mara yake ya kwanza kufanyiwa kitendo hicho.

MTOTO ANENA
Mtoto huyo akiongea na NIPASHE alisema kabla ya kufanyiwa unyama huo, mtuhumiwa huyo alikwenda kumchukua wakati akicheza na watoto wenzake.
"Nilikuwa nacheza alikuja Mgosi na kunichukua hadi chumbani kwake na kunilalia juu, kila siku ananifanyia hivyo na kuniambia nisiseme kwa mtu atanipiga," alisema mtoto huyo.
Alisema siku ya mwisho mtuhumiwa huyo mara baada ya kumaliza haja zake alimwambia arudi nyumbani kwao haraka.
"Nilirudi nyumbani niliogopa mama atanikuta nikitoka kwa mgosi, lakini niliona maumivu makali," aliongeza kusema.

POLISI WAMKAMATA
MTUHUMIWA
Baba mzazi wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alisema tukio waliliripoti kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusufu baada ya kumaliza taratibu zote za kumpatia matibabu Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.
Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kukaa ndani kwa siku kumi, kisha kuachiwa kwa dhamana.
Hata hivyo, alisema hajaridhishwa na mwenendo wa suala hilo baada ya polisi wa kituo hicho kumzungusha kwa muda mrefu na hakuna dalili ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.
"Tumekatishwa tamaa na utendaji wa polisi, hivi sasa imefikia muda wa mwezi mmoja hakuna kilichofanyika huku mtuhumiwa ameachiwa huru," alisema.
POLISI YATOA TAMKO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Camilius Wambura, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema halifahamu na kuahidi kulifuatilia kwa kina ili aweze kutolea ufafanuzi.
Hata hivyo, aliwataka wananchi kutambua wajibu wa jeshi hilo siyo tu kumfikisha mahakamani mtuhumiwa, badala yake inawajibika kufanya upelelezi kisha jalada husika kulipeleka kwa mwanasheria wa serikali kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
"Naomba wananchi wafahamu kwamba polisi kazi yao ni kupeleleza tu, kazi ya kufikisha mahakamani ni Ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali (DPP), hivyo kutupa lawama ni kutuonea," alisema Kamanda Wambura.
Alisema hata suala la mtu kupewa dhamana lipo kisheria na kila mtu ana haki ya kudhaminiwa, bali kwa makosa machache ya jinai kama kuua, wizi wa matumizi ya nguvu, biashara ya madawa ya kulevya ndiyo mtuhumiwa wake hawezi kupewa dhamana.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI  
    source boss ngasa