Justin
Bieber ni msanii ambaye amekuwa katika vichwa vingi vya habari miezi
kadhaa ya karibuni, sio kwasababu ya kazi nzuri anayoifanya bali ni
kutokana na vurugu na uvunjaji wa sheria wa kupita kiasi, kiasi kwamba
hivi karibuni wananchi wa Marekani wamempigia kura (Deport Bieber
Petition) ya kuiomba serikali imrudishe kwao sababu wamechoshwa na tabia
zake.
Mke
wa Rais wa Marekani Michelle Obama ametoa ushauri kwa wazazi wa msanii
huyo, akijitolea mfano kama yeye ndio angekuwa mzazi wa Bieber (19), kwa
kueleza kile ambacho angejaribu kufanya kumsaidia mwanaye katika
kipindi hiki ambacho ameonekana kuwa na changamoto nyingi zinazoonekana
kusababishwa na umri wake (foolish age).
First Lady amesema kama yeye angekuwa mzazi wa Bieber angejaribu kuwa naye karibu muda wote, na kuzungumza naye na kumshauri.
“Mimi ningekuwa karibu
naye sana kwenye maisha yake katika kipindi hiki….kuongea naye, ili
kujua nini kinaendelea katika kichwa chake, na kujua nani yuko katika
maisha yake na nani hayuko.” Alisema Michelle katika mahojiano ya hivi
karibuni na kituo cha Univision Radio.
Kuna uwezekano ushauri
wa first lady ni siri ya mafanikio ya malezi bora wanayoyapata mabinti
zake wawili Sasha na Malia, ambao pamoja kuwa ni watoto wa Rais wa taifa
kubwa duniani lakini wanaonekana kuwa na nidhamu.
”[Kids] just want you
near, you know — they want that advice from a parent. They want to see
you on a daily basis, because the thing is he’s still a kid. He’s still
growing up. So, I would pull him close.” Aliongeza Michelle.
Credit:Bongo5.com
Credit:Bongo5.com



























