
Hii
stori imekuja wakati Merkel na viongozi wengine wa Ulaya wanakutana
mjini Brussels kwa mkutano ambao unaonekana utagubikwa na habari za
mawasiliano ya siri yanayodaiwa kufanywa na Marekani kwa washirika wake
ambapo waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Thomas de Maiziere aliliambia
shirika la habari la ARD Ujerumani kwamba iwapo madai haya
yatathibitishwa kuwa ya kweli basi litakuwa ni jambo baya sana.
De Maiziere amesema Marekani itabakia kuwa rafiki wa Ujerumani lakini
jambo linalodaiwa kufanywa sio sahihi kabisa baada ya kupokea taarifa
kwamba Marekani ilifatilia mawasiliano ya kansela Angela Merkel hatua
iliomfanya Merkel mwenyewe Jumatano kumpigia simu mara moja rais wa
Marekani Barack Obama kutaka ufafanuzi zaidi kwa sababu aliamini kuna
siku mawasiliano yake yatafatiliwa lakini sio na Marekani.
Baada
ya haya madai ya Ujerumani, Marekani imekanusha kwa kusema
haijayachunguza mawasiliano ya Kansela na haiwezi kufanya hivyo kamwe.
Haya
madai yalitolewa kwa mara ya kwanza na mfanyakazi wa zamani wa idara ya
kitaifa ya usalama nchini Marekani, NSA, Edward Snowden yaliyochapishwa
na jarida la habari la Ujerumani, Der Spigel na sasa yameanza kuleta
uhusiano mbaya kati ya Marekani na mataifa ya Ulaya yaliyokasirishwa na
habari hizo za kufanyiwa uchunguzi wa siri na mshirika wao.

Mpaka
usiku wa October 24 2013, taarifa mbalimbali ziliripoti kwamba mpaka
sasa imefahamika ni viongozi wa nchi 35 kubwa wameshafatiliwa kwenye
mawasiliano yao ya simu za mkononi bila wenyewe kufahamu.
chanzo millad ayo
No comments:
Post a Comment