Friday, September 5, 2014

Inasikitisha sana angalia hapa picha za ajali iliyotokea Musoma picha zinatisha tafadhari

Watu 36 wamefariki dunia papohapo na wengine 79 kujerihiwa vibaya  katika  ajali  mbaya  ambayo imetokea  saa tano leo asbuhi katika kijiji cha sabasaba nje kidogo ya mji wa musoma  wilaya  ya butiama  mkoani mara  kwa kuhusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo aina ya Nissani Tellono  yenye  namba  za usajili T332 AKK. 
Mbali na gari hilo kugongwa na kutumbukia ndani ya mto mmoja katika daraja hilo kwenye barabara  kuu ya Musoma –Mwanza  pia mabasi  mawili  ambayo  yamehusika  katika  ajali  mbaya ni  j4 express  yenye namba za usali  T677 CYC liyokuwa ikitokea jijini Mwanza kwenda sirari  wilayani  tarime   ambalo  limegongano  uso  kwa uso  na  basi  la  Mwanza coach yenye namba T736 AWJ lilokuwa likitokea  Musoma kwenda jijini Mwanza.
Baada ya taarifa za ajali kusambaa katika manipaa ya  musoma  vilio na  simanzi  vimetawala  katika  mji huo wa Musoma mkoani Mara  baada majeruhi  na miili ya  marehemu  wa  ajali  hiyo  kuanza kufikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma.
Wakizungumza wakati  wakipatiwa matibabu  baadhi  ya  majeruhi  wa ajali hiyo   wamesema  kuwa  ajali hiyo imesababishwa  na  mwendo  kasi  wa mabasi   hayo  hatua ambayo ilisababisha kushindwa kupishana katika daraja hilo hivyo  kugongana uso kwa uso.
 akizungumza  kwa niaba  ya  mganga mkuu  wa  mkoa wa  Mara Dk Martin Khan,amesema  kuwa wamepokea maiti na idadi kubwa ya majeruhi  na wengi  wao hali  zao si za kuridhisha.
Hata hivyo  Dk  Khan  ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujitolea damu kwani amesema kuwa hospital  hiyo  ya  rufaa  ya  mkoa wa  mara inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu katika kuhudimia wagonjwa wakiwemo majeruhi wa ajali.
kamanda wa polisi mkoa wa  Mara ACP Alex Kalangi, akizungumza na ITV kwa njia  ya simu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba taarifa rasmi za jeshi la polisi zitatolewa baada ya kupata taarifa  kutoka kwa madaktari na  kwamba ametoa wito kwa  wananchi kujitokea katika hospitali ya mkoa  kwaajili ya kutambua miili ya marehemu.





No comments:

Post a Comment