Tatizo la Zitto sio ukanda, udini,
ukabila, usomi na siamini Waraka ambao wanasema Zitto anahusika
kwasababu umeandikwa kitoto sana.
Tatizo kubwa la Zitto na Chadema ni uhusiano binafsi na watu anaofanya nao kazi. Ukweli ni kwamba kazi ni zaidi ya sera, sheria za kwenye vitabu.
Viongozi wengi ni watu wa kawaida na wana uhusiano wa karibu hata wa kifamilia tumeona Kikwete analala kwa magufuli kwasababu Magufuli amegundua uhusiano binafsi ni njia moja wapo ya kufanikiwa kwenye jambo lolote. Hivyo Zitto hayo majungu yanatokana na kutokuaminiana kwasababu hujachukua muda kuweka mahusiano ya karibu na watu unaofanya nao kazi na hili ni tatizo kila mahali hata kwenye biashara au kazi nyingine.
Je unajua familia za wenzako, unajua wameamkaje asubuhi, unajua matatizo waliyonayo kama wagonjwa nyumbani? haya yote ni muhimu kwa watu unaofanyakazi nao sehemu moja. Vitabu vipo, sera zipo na sheria zipo lakini kwenye Chama kama Chadema ambacho ndicho kinakuwa na viongozi wachache kutupiana maneno kwenye mtandao inaonyesha hakuna mahusiano binafsi ambayo mnaweza kuongea kwenye chai ya asubuhi na kumaliza.
Hakuna jambo duniani linalofanikiwa kwa sera pekee bali mahusiano ni muhimu sana. Vilevile ni lazima uelewe mahusiano ni kati ya mambo muhimu ambayo ni lazima ukubali kama ni upungufu wako na kulifanyia kazi kama alivyofanya magufuli.
Magufuli pia alikuwa anaogopwa na JK na wengine kwa misimamo lakini aligundua hilo na kujenga mahusiano.
Zitto unakipaji na huna sababu ya kuwaeleza watu hilo kwasabbau kipaji ni kutoka kwa mungu na hakuna anayeweza kukichukua hivyo focus on your weakness.
Huu ni ushauri wangu kujibizana nani yuko sawa na nani hayuko sawa haitakusaidia popote pale na kwenye chama chocote au biashara.
Kitakacho kusaidia ni mahusiano-relationship
No comments:
Post a Comment